Thursday, 19 November 2015

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI - (Re-Advertised)




Tupo karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Plot No. 214, Boma Road
P.o. Box 4664 Morogoro, TANZANIA.

Simu: 0783400701 ama
0714022038

Email: Happyvalleyschools@gmail.com



TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Happy Valley Day Care Center iliyopo Morogoro mjini karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro inatangaza nafasi (1) ya kazi ya mwalimu wa elimu ya awali.


Majukumu ya mwalimu wa awali yatakuwa yafuatayo
· Kuwapokea watoto wafikapo shule na kuhakikisha wamerudi salama majumbani mwao
· Kuwafundisha watoto elimu ya awali
· Kuwahudumia watoto katika mahitaji yao mbalimbali
· Kuandaa michezo ya watoto na kuwasimamia wanapocheza
· Kutoa taarifa za watoto kwa wazazi kupitia shajara /diary za watoto
· Kuhakikisha usalama wa watoto wakati wote
· Kuhakikisha usafi wa watoto wakati wote
· Kuandaa ripoti za mitihani za watoto.
· Kufanya kazi nyingine yoyote ile inayoendana na taaluma ya elimu ya awali atakayoelekezwa na mkuu wake wa kazi.

Sifa za Muombaji
Awe anapenda watoto
Awe angalau na cheti cha ualimu wa elimu ya awali kutoka chuo kinachotambulika
Awe na uwezo wa kuongea na kuandika kwa ufasaha lugha ya Kiingereza na Kiswahili
Awe na umri usiopungua miaka (25)
Awe mbunifu katika kuandaa michezo ya watoto
Awe na ujuzi wa kuwaelewa watoto kwa haraka
Awe na uwezo wa kujituma kuliko kuamrishwa

Mwenye uzoefu wa kufundisha watoto atapewa kipaumbele


Tuma maombi yako kupitia anwani ya barua pepe (Email) inayoonekana hapo juu. Pamoja na barua yako ya maombi, ambatanisha wasifu wako (CV)  na nakala za vyeti vyako. Mwisho wa kutuma maombi ni tar 10/12/2015.

Kwa maelezo zaidi piga kupitia namba za simu zinaonekana hapo juu.