Una mwanao mwenye umri wa miaka miwili hadi sita? Unaishi Morogoro maeneo ya Area 5, Area 6, Kihonda, Kichangani, Msamvu, Nanenane ama eneo jingine lolote la Morogoro?
Unatafuta shule kwa ajili ya mwanao? Shule inayoaminika kwa malezi bora ya mtoto wako? Usalama wa mtoto akiwa shuleni? Chakula bora? Michezo bora?
Unahitaji mwanao ajengewe uwezo wa kujiamini, utu wema, uchapa kazi, kujitegemea, kupenda kujifunza na kadhalika?
Unahitaji kumwacha mwanao akiwa kwenye mikono ya walezi unaowaamini ambao wanataka kujenga urafiki kati yako, wao na mwanao?
Unahitaji mtoto wako awe shuleni lakini ajisikie yupo nyumbani?
Unahitaji mtoto wako afundishwe na walimu wenye hofu ya Mungu?
Kama umejibu ndiyo kwenye moja ya maswali hapo juu basi Happy Valley Day Care Center ni chaguo lako. Happy Valley Day Care Center ni shule mpya yenye walimu wazoefu iliyopo eneo la Boma karibu na ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro . Shule hii inakaribisha watoto wenye miaka miwili hadi mitano wajiandikishe tayari kwa muhula wa masomo utakaoanza Januari 2016.
Kwa mawasiliano zaidi tuandikie
Happyvalleyschools@gmail.com
No comments:
Post a Comment